Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Kumi na Nne · Usalama wa Kitaifa

Kifungu cha 242

Kif.242

Kubuniwa kwa Huduma ya Upelelezi ya Kitaifa

(1)Huduma ya Upelelezi ya Kitaifa imebuniwa.

(2)Huduma ya Upelelezi ya Kitaifa––

(a)Inawajibika katika upelelezi wa kiusalama na wa kuzuia tishio lolote kwa usalama ili kuboresha usalama wa kitaifa kulingana na Katiba hii; na

(b)hutekeleza majukumu mengine yoyote yaliyotolewa kwa mujibu wa sheria ya kitaifa.

Isome ndani ya Sura ya Kumi na Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho