Uongozi wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi
(1)Huduma za Polisi za Kitaifa imebuniwa.
(2)Huduma za Polisi za Kitaifa zinajumuisha—
(a)Huduma za Polisi wa Kenya; na
(b)Huduma za Polisi wa Utawala.
(3)Huduma za Polisi za Kitaifa ni huduma za kitaifa ambazo zitatekelezwa kote nchini Kenya.
(4)Bunge litatunga sheria ili kuwezesha utekelezaji wa Kifungu hiki kikamilifu.