Huduma ya Polisi ya Kitaifa
(1)Tume ya Huduma za Polisi za Kitaifa imebuniwa.
(2)Tume hiyo inajumuisha—
(a)watu wafuatao, kila mmoja wao akiwa ameteuliwa na Rais—
(i)mtu anayestahiki kuteuliwa kama Jaji wa Mahakama Kuu;
(ii)maafisa wawili wa polisi wa ngazi ya juu waliostaafu; na
(iii)watu watatu waadilifu ambao wamewahi kuhudumia umma kwa umahiri mkubwa;
(b)Inspekta-Jenerali wa Huduma za Polisi za Kitaifa; na
(c)Manaibu wote wawili wa Inspekta-Jenerali wa Huduma za Polisi za Kitaifa.
(3)Tume—
(a)itaajiri na kuteua watu ili kuhudumu au kutoa huduma kwa muda mfupi katika ofisi zilizo kwenye huduma hizo, itaidhinisha uteuzi na kuamua watakaopandishwa vyeo na kuhamishwa katika Huduma za Polisi za Kitaifa;
(b)itazingatia mchakato uliowekwa, itachukua hatua za kinidhamu na kuwaondoa watu wanaohudumu katika ofisi za Huduma hizo; na
(c)itatekeleza majukumu mengine yoyote yatakayotolewa kwa mujibu wa sheria ya kitaifa.
(4)Uajiri na uanachama katika Huduma za Polisi za Kitaifa utaonyesha utofauti wa kimaeneo na kikabila wa wananchi wa Kenya.