Kutumika kwa Sura
(1)Sura hii inatumika kwa tume zilizotajwa katika ibara ya (2) na ofisi huru zilizotajwa katika ibara ya (3), isipokuwa kwa kiwango ambacho Katiba hii inatoa mwongozo vinginevyo.
(2)Tume hizo ni—
(a)Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu na Usawa;
(b)Tume ya Kitaifa ya Ardhi;
(c)Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka;
(d)Tume ya Huduma za Bunge;
(e)Tume ya Huduma za Mahakama;
(f)Tume ya Ugavi wa Mapato;
(g)Tume ya Huduma za Umma;
(h)Tume ya Mishahara na Malipo;
(i)Tume ya Huduma kwa Walimu; na
(j)Tume ya Huduma za Polisi za Kitaifa.
(3)Ofisi huru ni—
(a)Mkaguzi Mkuu; na
(b)Msimamizi wa Bajeti.