Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nne · Sheria za Haki

Kifungu cha 29

Kif.29

Uhuru na usalama wa mtu

Kila mtu ana haki ya uhuru na usalama wake ambao inajumuisha haki ya—

(a)kutonyimwa uhuru kiholela au bila sababu;

(b)kutozuiliwa bila kushtakiwa mahakamani, isipokuwa wakati wa hali ya dharura, ambapo kuzuiliwa huko lazima kulingane na matakwa ya Kifungu cha 58;

(c)kuwa huru kutokana na aina yoyote ya ukatili kutoka kwa umma au watu binafsi;

(d)kutoteswa kwa njia yoyote, iwe kimwili au kisaikolojia;

(e)kutoadhibiwa kwa njia ya viboko; au

(f)kutotendewa au kuadhibiwa kwa njia ya kikatili, inayodhalilisha hadhi ya ubinadamu.

Isome ndani ya Sura ya Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho