Uhuru wa kujieleza
(1)Kila mtu ana haki ya uhuru wa kujieleza ambao unajumuisha—
(a)uhuru wa kutafuta, kupokea au kutoa maelezo au maoni;
(b)uhuru wa ubunifu wa kisanii; na
(c)uhuru wa kiakademia na utafiti wa kisayansi.
(2)Haki ya uhuru wa kujieleza haijumuishi—
(a)propaganda za vita;
(b)uchochezi unaozua ghasia;
(c)matamshi ya chuki; au
(d)utetezi kwenye misingi ya chuki ambao—
(i)unajumuisha uchochezi wa kikabila, kuwatusi wengine au uchochezi wa kusababisha madhara; au
(ii)unaotokana na misingi yoyote ya ubaguzi iliyotajwa au kubainiwa katika Kifungu cha 27 (4).
(3)Katika kutekeleza uhuru wa kujieleza, kila mtu ataheshimu haki na hadhi ya watu wengine.