Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nne · Sheria za Haki

Kifungu cha 36

Kif.36

Uhuru wa kutangamana

(1)Kila mtu ana haki ya uhuru wa kutangamana ambao unajumuisha haki ya kuanzisha, kujiunga na, au kushiriki katika shughuli za muungano wa aina yoyote.

(2)Mtu hatalazimishwa kujiunga na shirika la aina yoyote.

(3)Sheria yoyote inayohitaji usajili wa shirika la aina yoyote itaeleza kwamba—

(a)usajili huo hauwezi kuzuiwa au kuondolewa bila sababu maalum; na

(b)kutakuwepo haki ya kusikizwa kwa usawa kabla ya usajili huo kufutiliwa mbali.

Isome ndani ya Sura ya Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho