Mazingira
(1)Kila mtu ana haki ya mazingira safi na yenye afya, ambayo inajumuisha haki ya—
(a)mazingira kutunzwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo kupitia kwa hatua za kisheria na nyinginezo, hasa zile ambazo zinakusudiwa katika Kifungu cha 69; na
(b)majukumu yanayohusiana na mazingira kutimizwa chini ya Kifungu cha 70.