Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nne · Sheria za Haki

Kifungu cha 43

Kif.43

Haki za kiuchumi na za kijamii

(1)Kila mtu ana haki ya—

(a)kupata kiwango cha juu zaidi kiwezekanacho cha afya, kinachojumuisha haki ya huduma za kiafya ikijumuisha huduma ya afya ya uzazi;

(b)kupata makazi yanayofaa, na viwango vinavyostahili vya usafi;

(c)kuwa huru kutokana na njaa, na kupata chakula cha kutosha na bora;

(d)kupata maji safi na salama kwa viwango vinavyostahili;

(e)usalama wa kijamii; na

(f)elimu.

(2)Serikali itatoa ulinzi wa kijamii unaofaa kwa watu ambao hawawezi kujisimamia wao wenyewe pamoja na wanaowategemea.

Isome ndani ya Sura ya Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho