Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nne · Sheria za Haki

Kifungu cha 51

Kif.51

Haki za watu walio kizuizini, waliokamatwa au waliofungwa gerezani

(1)Mtu yeyote aliyezuiliwa, kukamatwa au kufungwa gerezani kisheria, ana haki zote na uhuru wote wa kimsingi katika Haki za Sheria, isipokuwa iwe kwamba haki au uhuru wowote wa kimsingi hauambatani kamwe na hali kuzuiliwa, kukamatwa au kufungwa gerezani kwa mtu huyo.

(2)Mtu aliyezuiliwa au kukamatwa ana haki ya kuwasilisha ombi la kutolewa kwa amri ya yeye kufikishwa mahakamani.

(3)Bunge litatunga sheria ambayo––

(a)inaagiza kuwa walio kizuizini, waliokamatwa au waliofungwa gerezani wapewe hadhi yao ya kibinadamu; na

(b)inazingatia mikataba ya kimataifa inayohusiana na haki za binadamu.

Isome ndani ya Sura ya Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho