Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nne · Sheria za Haki

Kifungu cha 56

Kif.56

Jamii za watu wachache na za watu waliotengwa

Serikali itaweka programu za hatua sawazishi zilizokusudiwa kuhakikisha kwamba vikundi vya watu wachache waliotengwa na kubaguliwa—

(a)vinashiriki na kuwakilishwa katika uongozi na katika nyanja zote za maisha;

(b)vinapewa nafasi maalum katika nyanja za elimu na uchumi;

(c)vinapewa nafasi maalum katika upataji wa ajira;

(d)vinakuza tamaduni zao, lugha na desturi zao; na

(e)vinapata maji, huduma za afya na miundombinu.

Isome ndani ya Sura ya Nne →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho