Wazee katika jamii
Serikali itachukua hatua ili kuhakikisha haki za wazee––
(a)kushiriki kikamilifu katika masuala ya jamii;
(b)kufuatilia ustawi wao wa kibinafsi;
(c)kuishi katika hadhi na heshima na kuwa huru kutokana na dhuluma; na
(d)kupata malezi ya kufaa na msaada kutoka kwa familia zao na Serikali.