Jukumu la Bunge la Kitaifa
(1)Bunge la Kitaifa linawakilisha watu walio katika maeneobunge na walio na maslahi maalum katika Bunge la Kitaifa.
(2)Bunge la Kitaifa hushauriana kuhusu maswala yenye umuhimu kwa wananchi na kuyasuluhisha.
(3)Bunge la Kitaifa hutunga sheria kwa kuzingatia Sehemu ya 4 ya Sura hii.
(4)Bunge la Kitaifa––
(a)huamua jinsi ya kugawa mapato ya kitaifa kati ya ngazi za Serikali, kama inavyobainishwa katika Sehemu ya 4 ya Sura ya Kumi na Mbili;
(b)hugawa fedha kwa matumizi ya serikali ya kitaifa na vitengo vingine vya Serikali vya kitaifa; na
(c)(c) hufuatilia uwajibikaji katika mapato ya kitaifa pamoja na matumizi yake.
(5)Bunge la Kitaifa—
(a)hukagua utendakazi katika ofisi ya Rais, ya Naibu Rais na maafisa wengine wa Serikali na huanzisha mchakato wa kuwaondoa ofisini; na
(b)hufuatilia uwajibikaji wa vitengo vya Serikali.
(6)Bunge la Kitaifa huidhinisha matangazo ya vita na kuongezwa kwa muda katika hali za hatari.