Jukumu la Seneti
(1)Seneti inawakilisha kaunti na inahudumu ili kulinda maslahi ya kaunti na ya serikali za kaunti hizo.
(2)Seneti hushiriki katika jukumu la Bunge la kutunga sheria kwa kutathmini, kujadiliana, kuidhinisha Miswada inayohusu kaunti, kama ilivyobainishwa katika Vifungu vya 109 hadi 113.
(3)Seneti huamua jinsi ya kugawa mapato ya kitaifa miongoni mwa kaunti kama ilivyobainishwa katika Kifungu cha 217, na hufuatilia uwajibikaji katika mapato ya kitaifa yaliyogawa katika serikali za kaunti.
(4)Seneti hushiriki katika uwajibikaji wa maafisa wa Serikali kwa kuzingatia na kutoa maamuzi kuhusu hoja ya kumwondoa Rais au Naibu wa Rais kutoka ofisini kulingana na Kifungu cha 145.