Uanachama wa Bunge la Kitaifa
(1)Bunge la Kitaifa linajumuisha—
(a)wabunge mia mbili tisini, kila mmoja wao akiwa amechaguliwa na wapigakura waliosajiliwa katika maeneobunge yanayotoa mbunge mmoja kwa kila eneobunge;
(b)wanawake arobaini na saba, kila mmoja wao akiwa amechaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa katika kaunti, kila kaunti ikiwa na eneobunge linalotoa mbunge mmoja;
(c)wabunge kumi na wawili walioteuliwa na vyama vya kisiasa vya bunge kulingana na idadi ya wabunge wa vyama hivyo katika Bunge la Kitaifa kwa mujibu wa Kifungu cha 90, ili kuwakilisha maslahi ya watu maalum ikijumuisha vijana, watu wenye ulemavu na wafanyakazi; na
(d)Spika, ambaye ni mwanachama aliyechaguliwa na wabunge.
(2)Hakuna chochote katika Kifungu hiki kinachoweza kufasiriwa kama cha kumzuia mtu yeyote katika kugombea uchaguzi chini ya ibara ya (1) (a).