Katiba ya Kenya, 2010

Sura ya Nane · Mabunge

Kifungu cha 98

Kif.98

Uanachama wa Seneti

(1)Seneti inajumuisha—

(a)wanachama arobaini na saba, kila mmoja wao akiwa amechaguliwa na wapiga kura waliosajiliwa katika kaunti, na kila kaunti ikiwa na eneobunge linalowakilishwa na mbunge mmoja;

(b)wanawake kumi na sita watakaoteuliwa na vyama vya kisiasa kulingana na idadi ya maseneta wao katika Seneti waliochaguliwa chini ya ibara ya (a) kulingana na Kifungu cha 90;

(c)wanachama wawili, wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja, wanaowawakilisha vijana;

(d)wanachama wawili, wakiwa mwanamume mmoja na mwanamke mmoja, wanaowawakilisha watu wenye ulemavu; na

(e)Spika, ambaye atakuwa mwanachama aliyechaguliwa na maseneta katika Seneti.

(2)Wanachama waliotajwa katika ibara ya (1) (c) na (d) watachaguliwa kulingana na Kifungu cha 90.

(3)Hakuna chochote katika Kifungu hiki kinachoweza kufasiriwa kama cha kumzuia mtu yeyote katika kugombea uchaguzi chini ya ibara ya (1) (a).

Kwenye kura yako ya 2027

Kifungu hiki kinahusu chaguzi hizi

Isome ndani ya Sura ya Nane →

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho