Maadili na kanuni katika huduma kwa umma
(1)Maadili na kanuni za huduma kwa umma zinajumuisha—
(a)viwango vya juu vya maadili ya kitaaluma;
(b)matumizi ya rasilimali kwa njia bora, ya kiuchumi na yenye ufanisi;
(c)utoaji huduma kwa njia inayokabiliana na hitaji, kwa haraka, kwa njia yenye ufanisi na usiokuwa na mapendeleo;
(d)kushirikishwa kwa wananchi katika mchakato wa kutengeneza sera;
(e)uwajibikaji katika hatua za kiutawala;
(f)uwazi na utoaji wa maelezo yaliyo sahihi na kwa wakati ufaao kwa umma;
(g)kwa kuzingatia aya za (h) na (i), ushindani wenye usawa na ustahiki kuwa misingi ya kuteuliwa na kupandishwa cheo;
(h)uwakilishi wa jamii tofauti za Kenya; na
(i)kutoa nafasi za kutosha na zenye usawa katika kuteua, kutoa mafunzo na kupandishwa vyeo katika ngazi zote za huduma kwa umma, kwa––
(ii)wanaume na wanawake;
(iii)watu wa jamii zote; na
(iv)watu wenye ulemavu.
(2)Maadili na kanuni za huduma za umma zinatumika kwa huduma za umma katika—
(a)vitengo vyote vya Serikali katika viwango vyote viwili vya serikali; na
(b)mashirika yote ya Serikali.
(3)Bunge litatunga sheria ili kuwezesha utekelezaji wa Kifungu hiki kikamilifu.