(1)Iwapo mtu amepata uraia kwa kusajiliwa, uraia huo unaweza kufutiliwa mbali ikiwa mtu huyo––
(a)alipata uraia huo kwa njia ya ulaghai, udanganyifu au kuficha ukweli wa maelezo yoyote husika;
(b)alifanya biashara isiyo halali au kuwasiliana na adui wakati wa vita ambavyo Kenya ilihusika, amejihusisha au kushiriki katika biashara ambayo ilifanywa kwa njia ya kumsaidia adui katika vita hivyo;
(c)katika kipindi cha miaka mitano baada ya kusajiliwa, amepatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu au zaidi; au
(d)kwa wakati wowote ule baada ya kusajiliwa, amepatikana na hatia ya uhaini au hatia ambayo––
(i)hukumu ya angalau miaka saba gerezani inaweza kutolewa; au
(ii)hukumu kali zaidi inaweza kutolewa.
(2)Uraia wa mtu ambaye alichukuliwa kuwa raia kwa kuzaliwa, kama inavyobainiwa katika Kifungu cha 14 (4), unaweza kufutiliwa mbali ikiwa–
(a)uraia huo ulipatikana kwa njia ya ulaghai, udanganyifu au kwa kuficha ukweli wa maelezo yoyote husika;
(b)uraia au kuzaliwa kwa mtu huyo kunajulikana na kunafichua kwamba mtu huyo alikuwa raia wa nchi nyingine; au
(c)umri wa mtu huyo unajulikana na unafichua kwamba alikuwa na umri wa zaidi ya miaka nane alipopatikana nchini Kenya.