Katiba ya Kenya, 2010

Utangulizi

Maneno ya mwanzo: nani anatoa Katiba hii, na kwa nini.

Sisi, watu wa Kenya,

TUNATAMBUA ukuu wa Mwenyezi Mungu muumba wa vyote:

TUNAWAHESHIMU mashujaa waliojitoa mhanga kuleta uhuru na haki nchini mwetu:

TUNAJIVUNIA tofauti zetu za kikabila, kitamaduni na kidini na tukiazimia kuishi kwa amani na umoja tukiwa taifa moja huru:

TUNATHAMINI mazingira, ambayo ndiyo urithi wetu na tukiazimia kuyadumisha kwa manufaa ya vizazi vijavyo:

TUNAJITOLEA kukuza na kuhifadhi maslahi ya mtu binafsi, familia, jamii na taifa:

TUNATAMBUA matarajio ya Wakenya wote ya serikali iliyo na misingi bora ya maadili ya haki za binadamu, usawa, uhuru, demokrasia, haki za kijamii na utawala wa kisheria:

TUNATUMIA uhuru wetu na haki yetu ya kuamua aina ya uongozi katika nchi yetu na tukiwa tumeshiriki kikamilifu katika kuiunda Katiba hii: TUNAIKUBALI,

TUNAIPITISHA, na kujipatia sisi wenyewe na vizazi vijavyo, Katiba hii.

MUNGU IBARIKI KENYA

Maandishi: Tafsiri ya Kiswahili ya Katiba ya Kenya, 2010, iliyochapishwa na Uraia kwa kutumia chapisho la Halmashauri ya Kitaifa ya Kuripoti Maswala ya Sheria (27 Agosti 2010). Ikiwa kuna utata wowote kuhusu tafsiri, nakala ya Kiingereza ndiyo rasmi.

Huu ni msaada wa kusoma, si ushauri wa kisheria. Kwa swali la kisheria, ongea na wakili. Umeona kosa? Ripoti marekebisho