Mahusiano ya kikazi
(1)Kila mtu ana haki ya hatua na desturi za kikazi zilizo na usawa.
(2)Kila mfanyakazi ana haki ya—
(a)kulipwa kwa haki;
(b)mazingira ya kikazi yanayofaa;
(c)kuunda, kujiunga au kushiriki katika shughuli na mipango ya chama cha wafanyakazi; na
(d)kugoma.
(3)Kila mwajiri ana haki ya—
(a)kuunda au kujiunga na shirika la waajiri; na
(b)kushiriki katika shughuli na mipango ya shirika la waajiri.
(4)Kila chama cha wafanyakazi na chama cha waajiri kina haki ya—
(a)kuamua usimamizi wake, mipango na shughuli zake;
(b)kupanga; na
(c)kuunda na kujiunga na chama cha wafanya kazi.
(5)Kila chama cha wafanyakazi, shirika la waajiri na mwajiri ana haki ya kushiriki katika maafikiano ya pamoja.