Watoto
(1)Kila mtoto ana haki ya––
(a)kupata jina na uraia wakati anapozaliwa;
(b)kupata elimu ya kimsingi na ya lazima bila malipo;
(c)kupata lishe bora ya kimsingi, makazi na huduma za afya;
(d)kulindwa kutokana na dhuluma, kutelekezwa, tamaduni mbaya zinazoathiri, aina zote za ukatili, matendo na adhabu zisizo na ubinadamu, na kazi yoyote ya kunyanyasa au yenye kuhatarisha;
(e)kutunzwa na kulindwa na wazazi, ambayo inajumuisha wajibu sawa wa mama na baba katika kukidhi mahitaji ya mtoto, bila kujalisha ikiwa wameoana au hawajaoana; na
(f)kutozuiliwa, isipokuwa wakati ambapo hilo ndilo hatua pekee inayoweza kuchukuliwa, azuiliwe––
(i)kwa muda mfupi zaidi unaostahili; na
(ii)kwa kutenganishwa na watu wazima na katika hali inayozingatia umri na jinsia ya mtoto huyo.
(2)Maslahi mema zaidi ya mtoto ni muhimu sana katika kila suala linalomhusu mtoto.