Watu wenye ulemavu
(1)Mtu mwenye ulemavu wowote ana haki ya––
(a)kupewa hadhi yake na heshima na kuzungumziwa na kutajwa kwa njia isiyomdunisha;
(b)kufikia taasisi za elimu na vifaa vya watu wenye ulemavu vilivyowekwa katika jamii kwa kiwango kinachoambatana na maslahi ya mtu huyo;
(c)kufikia ipasavyo maeneo yote, usafiri wa umma na habari au maelezo;
(d)kutumia lugha ya ishara, Breli, au njia nyingine mwafaka ya mawasiliano; na
(e)kupata nyenzo na vifaa vinavyoweza kumsaidia kukabiliana na matatizo ya ulemavu huo;
(2)Serikali itahakikisha utekelezaji unaoendelea wa kanuni kwamba, angalau asilimia tano ya watu walio katika mashirika ambayo wanachama huchaguliwa au kuteuliwa ni watu wenye ulemavu.