

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

ZAIDI ya wakulima 700,000 wa majanichai wanatarajiwa kupokea malipo ya bonasi ya kila mwaka leo, huku fedha hizo zikiingia katika akaunti zao pamoja na malipo ya kawaida ya mwezi Septemba.
Mwenyekiti wa Mamlaka ya Kilimo cha Majanichai (KTDA) Enos Njeru, alisema fedha hizo zilitolewa Ijumaa kwa hivyo wakulima watazipokea kwenye benki leo.