Kazi na mamlaka ya kijumla
(1)Kila tume, na kila anayehudumu katika ofisi huru—
(a)anaweza kufanya uchunguzi kwa kuchukua hatua hiyo kivyake au kwa malalamishi yaliyotolewa na mwananchi;
(b)ana mamlaka yanayohitajika katika upatanishina mazungumzo kwa madhumuni ya kutatua mzozo;
(c)atawaajiri wafanyakazi wake; na anaweza kutekeleza majukumu na mamlaka mengine yoyote yaliyotolewa kwa mujibu wa sheria, zaidi ya majukumu na mamlaka yaliyotolewa na Katiba hii.
(2)Malalamishi kwa tume au kwa anayehudumu katika ofisi huru yanaweza kuwasilishwa na mtu yeyote ambaye ana haki ya kuwasilisha kesi mahakamani chini ya Kifungu cha 22 (1) na (2).
(3)Tume na ofisi huru zifuatazo zina mamlaka ya kumwita shahidi ili kutoa usaidizi kwa madhumuni ya uchunguzi wa tume au ofisi hiyo—
(a)Tume ya Kitaifa ya Haki za Binadamu na Usawa;
(b)Tume ya Huduma za Mahakama;
(c)Tume ya Kitaifa ya Ardhi;
(d)Mkaguzi Mkuu.