Image: Taifa LeoViongozi maarufu wa siasa wavua vazi la heshima na kurushina majina ya kudhalilishana
Published on November 11, 2026
SIASA za Kenya zinazidi kutawaliwa na vijembe, majina ya kejeli na mashambulizi binafsi huku viongozi wakionekana kutumia muda mwingi kushambuliana badala ya kueleza mipango yao ya kuboresha maisha ya wananchi. Mvutano huo umeongezeka kati ya Rais William Ruto na aliyekuwa naibu wake Rigathi Gachagua, huku kila mmoja akimtupia mwenzake tuhuma na majina ya kumdhalilisha kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.





