

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

KAKAKE marehemu mwanamuziki maarufu wa nyimbo za injili Betty Bayo, amekata kauli na kusema hataifuatilia tena kesi inayochunguza kiini cha kifo cha dada yake.
“Sasa nimejiridhisha kwamba dadangu alifariki kutokana na kuugua AMN. Hii ni baada ya uchunguzi wa kina wa kimatatibabu kufanywa kuhusu kiini cha kifo chake. Nimeridhika na sasa nitamwacha dadangu apumzike kwa amani,” alisema ndugu huyo Edward Mbugua.