

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →
Party activity

KIONGOZI wa chama cha Democracy for the Citizens (DCP) Rigathi Gachagua anadai analenga kuunganisha viongozi wa upinzani chini ya mgombeaji mmoja wa urais katika uchaguzi wa 2027, lakini matamshi yake makali dhidi ya washirika wake yameibua wasiwasi.
Bw Gachagua anaendelea kuwakosoa baadhi ya vinara wa upinzani akiwalaumu kwa kutofanya bidii kujenga umaarufu, huku akisisitiza kuwa hakuna mtu atakayekabidhiwa urais bila kuungwa mkono na wapigakura.