

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →
Party activity

KATIBU Mkuu wa chama cha UDA Hassan Omar ameitaka Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kutupilia mbali malalamishi dhidi yake kuhusu kauli aliyotoa kuwa hata watu waliokufa wanaweza kupiga kura katika uchaguzi mkuu wa 2027.
Omar alisema matamshi hayo aliyotoa Septemba 11 yalikuwa mzaha wa kisiasa uliolenga kuwahamasisha wakazi wa Pwani kujisajili kama wapigakura na kushiriki uchaguzi, wala si wito wa kufanya udanganyifu.