

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

WANAHARAKATI wamepoteza kesi ya kutaka wananchi waruhusiwe kufanya maandamano nje ya Ikulu na ikulu ndogo ya Rais katika maeneo mbalimbali nchini.
Mahakama ilitupilia mbali kesi iliyowasilishwa na kundi la Operation Linda Jamii, ikisema halikuthibitisha jinsi notisi zilizotangaza makazi hayo kuwa maeneo yaliyolindwa zinavyokiuka Katiba au sheria.