

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →
Election process

MASHIRIKA matatu ya kutetea haki za binadamu yamewasilisha kesi katika Mahakama Kuu yakitaka serikali iunde jopokazi la mashirika mbalimbali ndani ya siku 30 kuchunguza na kuwafungulia mashtaka wanaohusika na ghasia za kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2027.
Mashirika hayo ni Kenya Human Rights Commission (KHRC), Katiba Institute na Independent Medico-Legal Unit (IMLU).