

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

MWANAMKE aliyemfikisha mumewe wa miaka 30 mahakamani ameshinda fidia ya Sh500,000 baada ya kuthibitisha kuwa hatua ya mumewe kumleta mwanamke mwingine katika nyumba yao ya ndoa ilikiuka haki zake za kikatiba.
Jaji wa Mahakama Kuu, Alfred Mebeya aliamua kuwa mwanaume huyo, GOB, alikiuka utu wa mkewe, BAC, kwa kumleta mpenziwe, FC, katika nyumba yao ya ndoa iliyoko Kombewa, Kaunti ya Kisumu.