Serikali ya Sakaja yafyonza Sh125 bilioni miradi ikikwama

Election

Source: Taifa LeoBy Fatuma Bariki👁 2 views

Johnson Sakaja

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

GAVANA wa Nairobi, Johnson Sakaja, aliingia ofisini mwaka wa 2022 akiwa na ahadi kubwa ya kuhakikisha kuwa mambo yanaenda sambamba Nairobi lakini miaka minne baadaye takwimu za matumizi ya fedha za umma zinaibua swali iwapo jiji hilo limetimiza lengo hilo.

Bw Sakaja alipokuwa akihutubu wakati wa kuapishwa kwake Agosti 2022, alikumbuka maisha yake ya utotoni Ngara na jinsi alivyoshangaa kuona baadhi ya mitaa ikiwa safi, yenye barabara nzuri na iliyopangwa huku mingine ikiwa katika hali mbaya.Alisema akiwa na umri wa miaka saba aliwahamasisha watoto wenzake kuandamana wakitaka mazingira yao yaimarishwe.


Author: Fatuma Bariki
Source: Taifa Leo

Read Full Article at Taifa Leo