

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

SERIKALI imesema imefaulu kwa asilimia 99 kuwafuatilia watu waliotagusana na mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini pamoja na jamaa zao, huku idadi ya visa vilivyothibitishwa vikifikia saba.
Kati ya visa hivyo, vinne ni vya watu ambao tayari walikuwa wametengwa kwa ajili ya kufuatiliwa. Maambukizi hayo yamesababisha kifo kimoja hadi sasa.