
Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

SENETA wa Nairobi Edwin Sifuna na baadhi ya viongozi wa Linda Mwananchi wamewakosoa baadhi ya viongozi wa ODM kwa kumkosea heshima mjane wa Raila Odinga, Mama Ida pamoja na familia ya waziri huyo mkuu wa zamani.
Akizungumza katika ibada ya kanisa, eneobunge la Embakasi Mashariki jana, Bw Sifuna alisema kuvurugwa kwa maadhimisho ya kwanza ya kifo cha Raila eneo la Bondo kulipangwa na viongozi wa eneo hilo waliopinga mwaliko wa viongozi wa Linda Mwananchi.