

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

WATAALAM wa afya wameitaka Wizara ya Afya kuharakisha msako wa watu 15 ambao hawajapatikana, licha ya kuwa miongoni mwa watu 128 waliotangamana na mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini Kenya.
Wizara ilisema kufikia Oktoba 13, watu 113 walikuwa wamepatikana, wakiwemo 108 waliowekwa karantini nchini Kenya na wengine watano walio nje ya nchi. Haijafichua waliko watu 15 ambao hawajapatikana.