Uhuru wa Mahakama
(1)Katika utekelezaji wa mamlaka ya mahakama, Kitengo cha Serikali Kinachosimamia Mahakama, kama kilivyobuniwa chini ya Kifungu cha 161, kitazingatia Katiba hii na sheria, na hakitadhibitiwa wala kuelekezwa na mtu au mamlaka yoyote.
(2)Afisi ya jaji wa mahakama iliyo katika ngazi ya juu haitafutiliwa mbali wakati ambao kuna afisa anayehudumu katika afisi hiyo.
(3)Mishahara na marupurupu ambayo majaji wanalipwa yatatoka katika Hazina Jumuishi.
(4)Kwa kuzingatia Kifungu cha 168 (6), mishahara na marupurupu ambayo jaji anapaswa kulipwa, hayatabadilishwa kwa njia itakayomwathiri, na manufaa ya kustaafu ya jaji aliyestaafu hayatabadilishwa ili kumuathiri jaji huyo mstaafu katika maisha yake yote.
(5)Mwanachama wa mahakama hatawajibika katika hatua au kesi inayohusiana na chochote kilichofanywa au ambacho hakikufanywa kwa nia njema katika utendakazi wa kisheria majukumu ya mahakama yanapotekelezwa.