

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

SAFARI ya mbali huanza kwa hatua moja, ni kauli anayoienzi Francis Thoya ambaye hutengeneza vitafunwa kwa kutumia bidhaa za kula ambazo huishia kutupwa kwa wasioona thamani yazo.
Kilichoanza kwa kuchakata kilo moja ya vitafunwa vya samaki kwa jiko dogo kimestawi na kuwa biashara inayounganisha wakulima kupitia uongezaji thamani, huku ikilenga kukabiliana na changamoto za lishe eneo la Pwani.