Gavana akana dai hofu ya uchawi ilimfukuza ofisini

Source: Taifa LeoBy Fatuma Bariki👁 3 views

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

GAVANA wa Tana River, Bw Dhadho Godhana, ameeleza sababu zinazomfanya kutotumia mara kwa mara ofisi yake rasmi mjini Hola, na badala yake kufanyia kazi katika maeneo mengine, yakiwemo afisi za mahusiano ya nje ya kaunti yake zilizo mjini Mombasa na Nairobi.

Bw Godhana alipuuzilia mbali madai kwamba hofu ya uchawi ndiyo iliyomlazimu kuachana na ofisi yake ya Hola, akifafanua kuwa kufanya kazi kutoka maeneo mengine ni mkakati wa kudhibiti umati wa watu na kuhakikisha usalama.


Author: Fatuma Bariki
Source: Taifa Leo

Read Full Article at Taifa Leo