
Originally published by Taifa Leo — Read the original article →
Party activity

Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amejipata katikati ya vita vya kisiasa katika Mlima Kenya tangu alipotangaza azma ya kuwania urais, akipuuza chama cha UDA na kujiunga na People’s Party of Kenya (PPK).
Mbunge huyo anayehudumu muhula wa pili amekuwa akishambuliwa na washirika wa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, ambao wanadai ni kibaraka wa serikali ndani ya upinzani, anayetaka kugawanya kura za eneo la Mlima Kenya.