

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →
Party activity

Mvutano unaanza kutokota ndani ya chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP) kinachoongozwa na aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua, huku baadhi ya wanasiasa wanaotaka tiketi za chama hicho wakihofia kuwa viongozi fulani wanapendelewa kabla ya uchaguzi wa mchujo.
Wagombea hao wanadai kuwa licha ya kuahidiwa usawa kushindania tiketi, baadhi ya wapinzani wao wanaonekana kuwa na uungwaji mkono wa moja kwa moja kutoka kwa kiongozi wa chama na washirika wake wa karibu.