
Originally published by Taifa Leo — Read the original article →
Party activity

Aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua anajaribu kujenga muungano mpana wa upinzani utakaompa nafasi muhimu katika uchaguzi wa urais wa 2027. Hata hivyo, mpango wake wa kuunganisha maeneo yenye kura nyingi unakabiliwa na mvutano kuhusu nani atakayeongoza, nani atakayetoa kura na ni nani atakayekuwa na usemi mkubwa katika kugawana mamlaka.
Kutoka nyumbani kwake Wamunyoro, kiongozi huyo wa Democracy for the Citizens Party (DCP) anauza ujumbe wa mashauriano, ushirikiano na umoja wa upinzani. Lakini nyuma ya ujumbe huo kuna mkakati mkali unaoitwa Operation Okoa Kenya, unaolenga kuunganisha maeneo yenye ushawishi wa kisiasa, kupunguza ushawishi wa Rais William Ruto na kuwalazimisha wapinzani kujadiliana wakiwa na nguvu za kutosha.