

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

SAFARI ya walimu kutoka Kaunti ndogo ya Matete, Kaunti ya Kakamega, kuenda kusherehekea harusi ya mtoto wa mwenzao iligeuka msiba baada ya watu sita kufariki katika ajali ya barabarani.
Ajali hiyo ilitokea usiku wa manane wikendi karibu na Burnt Forest, kwenye barabara kuu ya Eldoret-Nakuru.