

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

BAYERN Munich na Paris Saint-Germain (PSG) zimeimarisha matumaini yao ya kutwaa taji la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) baada ya kupata ushindi mnono dhidi ya Atletico Madrid na Villarreal mtawalia Jumanne usiku.
Manchester United ilionyesha juhudi za kupambana kwa kurejea kutoka nyuma kwa mabao mawili na kuichapa AS Roma 3-2 katika mechi ya kusisimua kwenye Uwanja wa Old Trafford.