

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

BIASHARA za hoteli, Airbnb, mikahawa, teksi na uchuuzi zimepata msisimko mkubwa Eldoret huku wageni wakimiminika katika jiji hilo kuelekea kwenye sherehe za Mashujaa Dei zitakazoandaliwa leo katika Uwanja wa Kipchoge Keino.
Kuwasili kwa maafisa wa serikali, wajumbe wa kampuni na wageni wengine kumeongeza mahitaji ya malazi, chakula, usafiri na huduma nyingine, na kuwawezesha wafanyabiashara kuongeza mapato.