

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →
Party activity

JUHUDI za aliyekuwa Naibu wa Rais Rigathi Gachagua za kuunganisha eneo la Mlima Kenya chini ya chama chake cha Democracy for the Citizens (DCP) zinakabiliwa na changamoto mpya huku wanasiasa wengine wakitafuta nafasi katika siasa za upinzani kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027.
Kuibuka tena kisiasa kwa Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro, azma huru za Spika wa wa zamani wa Bunge la Kitaifa Justin Muturi na kiongozi wa Party of National Unity (PNU) Peter Munya, pamoja na kurejea kwa Martha Karua katika shughuli za upinzani, kunatishia kuvuruga mipango ya Bw Gachagua.