
Originally published by Taifa Leo — Read the original article →
Party activity

ODINGA Junior ameapa kubaki katika chama cha ODM na kumuunga mkono Rais William Ruto katika azma yake ya kuchaguliwa tena mwaka ujao, licha ya tofauti za kisiasa zinazozidi kujitokeza katika familia ya Odinga.
Jana, Raila Odinga Junior aliungana na viongozi wakuu wa ODM na Waziri wa Madini Hassan Joho katika mkutano wa kumbukumbu ya Raila Odinga uliofanyika Garissa.