

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

ZAIDI ya wanafunzi 261,000 waliotarajiwa kuendelea na masomo na kufanya mitihani ya kitaifa mwaka huu hawajulikani walipo, hali inayozua maswali kuhusu sera ya serikali ya kuhakikisha wanafunzi wote kutoka shule ya msingi wanajiunga na zile za sekondari.
Takwimu za Baraza la Kitaifa la Mitihani Kenya (KNEC) zinaonyesha kuwa watahiniwa 1,233,852 walifanya mtihani wa KCPE mnamo 2022.