

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →
Election process

VIONGOZI wa kisiasa wameanza kuhama vyama kwa wingi huku uchaguzi mkuu wa Agosti 10, 2027 ukikaribia, kila mmoja akitafuta tiketi ya chama anachoamini kitampa nafasi nzuri ya kushinda.
Katika siku za hivi majuzi, makao makuu ya vyama mbalimbali yamekuwa na shughuli nyingi, huku viongozi na wanasiasa wanaotaka kuwania nyadhifa tofauti wakipokelewa kutoka vyama pinzani.