

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

WAZAZI wanaendelea kutumia maelfu ya pesa kununua karatasi za mazoezi na mitihani ya kutabiri maswali yanayoweza kutokea katika mitihani ya kitaifa, hali inayoongeza mzigo kwa familia zinazokabiliwa na gharama kubwa ya maisha.
Biashara hiyo inahusisha karatasi za kutabiri maswali, mitihani ya majaribio, majibu na vikundi vya WhatsApp vinavyotoza ada kwa wanafunzi wanaotaka kujiandaa kwa mitihani.