

Originally published by Taifa Leo — Read the original article →

Kwa karibu miaka mitatu kuanzia mwishoni mwa 2019, mamia ya watu, wakiwemo watoto, walivutwa katika Msitu wa Shakahola, Kilifi, wakiamini wanaelekea kwenye maficho ya kiroho. Badala yake, eneo hilo liligeuka kuwa makaburi ya halaiki.
Kiini cha mkasa huo alikuwa mhubiri Paul Nthenge Mackenzie, ambaye mafundisho yake yaliwashawishi wafuasi kuacha makazi, kazi na maisha yao ya kawaida ili kujiandaa kwa kile alichodai kuwa ni mwito wa Mungu.